(*English printed below, please click 'read more')
Felix ni kijana mdogo wa miaka 15, anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Njiro Mkoani Arusha. Kijana huyu ameifahamu Twende kupitia utambulisho mfupi unaofanywa na wawakilishi kutoka kwenye kituo hiki cha ubunifu ambao hutembelea shule mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza na kuwafahamisha watu mbalimbali hasa wanafunnzi, nia na malengo ya kituo hiki ni kuwasaidia wabunifu wadogowadogo wenye mawazo ya kiubunifu na kuwawezesha kuyaweka katika uhalisia kwa lengo la kusuluhisha changamoto zinazo zisumbua jamii za kitanzania.
Katika kuwezesha wenye mawazo na ambao hawana mawazo tunatoa mafunzo ya takribani siku tatu ambapo wanajifunza ujuzi wa kutengeneza vitu kama vile tochi, chaja za simu kwa kutumia sola na kisha wanapewa nafasi ya kuja na changamoto ambayo ipo kwenye jamii walikotoka na kuitafutia ufumbuzi.
“Nilifurahi sana kuona wazo langu linafanya kazi na baada ya hapo nilipata ushawishi wa kuendelea kuifanyia kazi zaidi na zaidi ili nifikie malengo yangu.”
“Nilipendelea sana kuendelea kuja Twende kwa ajili ya kuendeleza mradi wangu kwa sababu ya ukarimu na msaada wa kiufundi na hata ushauri pamoja na vingine vingi nilivyovipata kutoka kwa watu wa Twende, pia baada ya wataalamu kuona na kudhibitisha kuwa wazo langu linaweza kufanya kazi ndipo namimi nilipata moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi Kwa kutengeneza mashine hii”
Felix alifurahi sana na kuona nae anaweza kuwa mbunifu kama wabunifu wengine na kisha kuisaidia jamii inayomzunguka na yeye mwenyewe.
Mawazo ya miradi mingine iliyokuzwa kutokana na mafunzo ya awamu hii ni pamoja na roboti ya kutembea kama mnyama, feni, kifaa cha kutobolea(drili) mkokoteni wa kutumia betri, mashine ya mazoezi inayochaji betri n.k.